Dante Alighieri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dante Alighieri jinsi alivyochorwa na Giotto wakati wa maisha yake

Dante Alighieri (14 Mei/13 Juni 1265 - 13/14 Septemba 1321) alikuwa mshairi bora wa lugha ya Kiitalia, mwenyeji wa mji wa Firenze, Italia.

Anasifiwa kama baba wa lugha ya Kiitalia akiwa mwanashairi maarufu wa kwanza aliyeandika kwa lugha ya watu badala ya Kilatini cha wataalamu na wasomi. Hutazamwa pia kama mshairi muhimu zaidi wa kipindi cha zama za kati za Ulaya.

Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.

Divina Commedia[hariri | hariri chanzo]

Kazi yake kuu ni shairi refu la Divina Commedia ambamo anatoa habari za safari yake ya kidhahania huko ahera akipitia jehanamu, toharani hadi paradiso. Ndiyo sehemu tatu za shairi lake zinazomwezesha kukiri imani yake ya Kikristo na kuchukua msimamo kuhusu watu na matukio hasa ya wakati wake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

De vulgari eloquentia, 1577

External links[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dante Alighieri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.