Waraka wa pili kwa Timotheo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya


Barua ya pili kwa Timotheo ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Ni moja ya kundi la Nyaraka za Kichungaji.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi ni Mtume Paulo akiwa kifungoni Roma kwa mara ya mwisho, muda mfupi kabla ya kukatwa kichwa wakati wa dhuluma (64-67 B.K.) ya Kaisari Nero dhidi ya Wakristo.

Maneno yake ya buriani yanaonyesha tumaini lake ambalo alikabili hicho kifodini.

Kiungo cha nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili