Waraka wa pili wa Petro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya


Barua ya pili ya Petro ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi[hariri | hariri chanzo]

Siku hizi wataalamu wanakubaliana kukanusha barua hiyo kuwa imeandikwa kweli na Mtume Petro, wakisema ni kitabu cha mwisho kuandikwa katika Agano Jipya (labda huko Roma mwaka 100 hivi B.K.).

Kwa hakika iliandikwa baada ya waraka wa Yuda, kwa sababu inatumia maneno yake mengi.

Inawezekana mwandishi alitumia vilevile maneno ya Petro ambayo sasa yamepotea; kwa vyovyote aliandika kwa mamlaka yake kwa makanisa yote ili kuthibitisha mapokeo.

Mada[hariri | hariri chanzo]

Pamoja na kupinga uzushi, lengo la barua ni kueleza sababu gani Bwana anachelewa kurudi.

Mafundisho mengine muhimu yaliyomo yanahusu uvuvio wa Roho Mtakatifu juu ya waandishi wa Biblia (Paulo mmojawao), wito wetu wa kushiriki umungu, uwepo wa ulimwengu mpya baada ya huu wa sasa kuangamizwa (2Pet 1:3-11,19 21; 3:8-18).


Kiungo cha nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili