Waraka kwa Wafilipi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya


Barua hiyo ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Katika Matendo ya Mitume Mwinjili Luka hakusimulia mateso yote ya Mtume Paulo, kwa mfano alivyohukumiwa mwaka 56 hivi Efeso (1Kor 15:32; 2Kor 1:8-9).

Akiwa kifungoni huko alifikiwa na mjumbe toka Filipi aliyemletea msaada wa pesa na wa huduma kwa niaba ya Wakristo wa mji huo.

Paulo kabla hajamrudisha alipenda kuwaandikia barua nzuri ya shukrani pamoja na kuwaeleza sababu ya kufungwa (Fil 4:10-20).

Barua ni nzuri pia kutokana na uhusiano wa upendo kati ya Paulo na Wakristo hao, ambao kati yao wanawake walishika nafasi ya pekee toka mwanzo.

Tunaona wazi Paulo alivyokuwa na furaha hata kifungoni, kwa kuwa alizoea kuridhika na kila hali: kwake muhimu ilikuwa tu kumfikia Yesu Kristo.

Kama kawaida mawaidha hayakosekani, lakini si makali: hasa alihimiza umoja kwa kufuata mfano wa Yesu aliyejishusha kutoka Umungu wake hadi kifo cha msalabani.

Kwa ajili hiyo alitumia maneno ya wimbo ambao unadhihirisha imani kamili katika umungu wa Kristo, ingawa ni kati ya zile za kwanzakwanza kutungwa (Fil 1:12-3:1a; 4:4-7).

Lakini kuna sehemu kali kuhusu wazushi ambayo inaanza ghafla (Fil 3:1b-4:1) na kufanya baadhi ya wataalamu wadhani kuwa barua jinsi ilivyo tangu karne I ni mshono wa barua mbili au tatu za mtume kwa Wafilipi.


Kiungo cha nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili