Lidia wa Thiatira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Lidia
Kikanisa cha Kiorthodoksi kilichojengwa mahali panaposemekana Lidia alibatizwa.

Lidia wa Thiatira (au Ludia wa Thuatira; kwa Kiingereza Lydia of Thyatira; kutoka Kigiriki Λυδία, jina la mkoa wa Dola la Roma ulikokuweko mji wa Thiatira, katika Uturuki wa leo[1]) alikuwa mwanamke mfanyabiashara wa karne ya 1[2] ambaye kwanza aliongokea dini ya Uyahudi[3][4].

Mwinjili Luka katika Matendo ya Mitume (kitabu cha Agano Jipya la Biblia ya Kikristo) alisimulia habari zake; hivyo amekuwa mtu wa kwanza wa Ulaya ambaye anajulikana kwa jina kuwa aliongokea Ukristo[5]. Ni tunda ambalo Mtume Paulo alilichuma huko Filipi (Ugiriki Kaskazini)[6].

Madhehebu mengi yanamheshimu kama mtakatifu katika tarehe tofautitofauti[7][8][9][10][11][12][13]. Kwa Wakatoliki wa Kanisa la Kilatini sikukuu yake ni tarehe 20 Mei[14] (awali 3 Agosti)[15].

Katika Matendo ya Mitume[hariri | hariri chanzo]

16:11 Basi tukang’oa nanga kutoka Troa, tukafika Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli; 12 na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. 13 Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. 14 Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo. 15 Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha.

Ndio ubatizo pekee katika Matendo ya Mitume ambao uliweza kufanyika katika maji mengi kutokana na mazingira (ujirani wa mto).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Cumming, John (1998). Butler's Lives of the Saints. Collegeville, MN: The Liturgical Press. uk. 24. 
 2. Ascough, Richard S. (2009). Lydia: Paul's Cosmopolitan Hostess. Collegeville, MN: The Liturgical Press. uk. 27. 
 3. Hahn, Scott (2002). The Acts of the Apostles Revised Standard Version (Second Catholic Edition). San Francisco, CA: Ignatius Press. uk. 45. 
 4. Cumming, John (1998). Butler's Lives of the Saints. Collegeville, MN: The Liturgical Press. uk. 25. 
 5. Cumming, John (1998). Butler's Lives of the Saints. Collgeville, MN: The Liturgical Press. uk. 24. 
 6. https://www.santiebeati.it/dettaglio/65200
 7. Ἡ Ἁγία Λυδία ἡ Φιλιππησία. 20 Μαΐου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ. (Kigiriki)
 8. St Lydia of Philippisia. OCA - Feasts and Saints.
 9. "St. Lydia of Philippisia". The Self-Ruled Antiochian Orthodox Christian Archdiocese of North America. 
 10. "St. Lydia of Thyatira: First Christian Convert in Europe, Deaconess of Philippi.". One Thing Needful (Monastery News). 
 11. "The Saints of God: Holy Women, Holy Men". Episcopal Life Weekly. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-02. Iliwekwa mnamo 2018-05-07.  More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)
 12. Kitahata, Stacy. "Bold Foremothers of Our Faith". Lutheran Woman Today. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-04-06. 
 13. Kinnaman, Scot A. (2010). Lutheranism 101. St. Louis: Concordia Publishing House. uk. 278. 
 14. Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana 2001 ISBN 978-88-209-7210-3), p. 278
 15. "St. Lydia Purpuria". 
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lidia wa Thiatira kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.