Filipi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ramani ya Ugiriki ikionyesha Filipi.

Filipi (kwa Kigiriki Φίλιπποι, Philippoi) ulikuwa mji wa Makedonia ya mashariki, ulioanzishwa na Filipo II wa Makedonia mwaka 356 KK ukaachwa katika karne ya 14 kutokana na uvamizi wa Waturuki.

Leo kuna Filippoi tena karibu na magofu ya mji wa zamani katika mkoa wa Makedonia ya mashariki and Thrakia nchini Ugiriki.

Vyombo vilivyopatikana Filipi.
Jina la askofu Porphyrios katika Basilika la Mt. Paulo.
Mabaki ya kanisa kuu.

Katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya Agano Jipya, mwaka 49 au 50 mji ulitembelewa na Mtume Paulo kutokana na njozi aliyoipata ikiwa na himizo la kuingia Ulaya ili kuwaletea Injili Wamakedonia (Mdo 16:9-10).

Paulo alidumisha uhusiano mzuri na jumuia ya Kikristo aliyoweza kuianzisha huko kwa muda mfupi, akaitembelea tena mwaka 56 na 57.

Waraka kwa Wafilipi uliweza kuandikwa miaka 61-62.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Ch. Bakirtzis, H. Koester (ed.), Philippi at the Time of Paul and after His Death, Harrisburg, 1998.
  • P. Collart, Philippes ville de Macédoine de ses origines jusqu'à la fin de l'époque romaine, Paris, 1937.
  • G. Gounaris, E. Gounaris, Philippi: Archaeological Guide, Thessaloniki, 2004.
  • P. Lemerle, Philippes et la Macédoine orientale à l'époque chrétienne et byzantine, Ed. De Boccard, Paris, 1945.
  • M. Sève, "De la naissance à la mort d'une ville : Philippes en Macédoine (IVe siècle av. J.-C.–VIIe siècle apr. J.-C.)", Histoire urbaine n° 1, juin 2000, 187–204.
  • Ch. Koukouli-Chrysanthaki, Ch. Bakirtzis, Philippi Athens, second edition, 1997.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Anwani ya kijiografia: 41°00′47″N 24°17′11″E / 41.01306°N 24.28639°E / 41.01306; 24.28639