Korintho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mahali pa Korintho

Korintho (Kigir.: Κόρινθος Kórinthos) ni mji wa Ugiriki ya Kusini. Iko kwenye shingo la nchi la Korinth linalounganisha rasi ya Peloponesi na Ugiriki bara.

Siku hizi ni mji mdogo tu mwenye wakazi 36,555 lakini ina historia kubwa na ndefu. Kimataifa Korintho inajulikana kutokana na mfereji wa Korintho unaokata shingo la nchi kwa urefu wa kilomita sita na kufupisha safari kutoka Adria kuingia Mediteranea ya mashariki kwa meli ndogo na za wastani.

Mfereji wa Korintho unavyokata shingo la nchi

Kihistoria jina la mji lajulikana zaidi kutoka Biblia na hasa barua za Mtume Paulo kwa Wakristo mjini zinazopatikana katika Agano Jipya kama Waraka wa kwanza kwa Wakorinto (1Kor.) na Waraka wa pili kwa Wakorinto (2.Kor.).

Kitovu cha biashara zamani za Ugiriki wa Kale[hariri | hariri chanzo]

Zamani za Ugiriki wa Kale Korintho ilikuwa bandari muhimu. Mji ulitajirika kutokana na biashara iliyopita kwenye shingo la nchi. Biashara yote kwa majahazi kati ya Italia na Asia Ndogo ilipita humo; bidhaa zilitolewa Korintho na kubebwa njia ya shingo la nchi hadi kuendlea kwa jahazi nyingine upande wa mashariki. Uwezo wake wa kiuchumi na kisiasa ulishindana na Atheni na Theben.

Mji wa Kiroma[hariri | hariri chanzo]

Mji uliharibiwa kabisa na Waroma mwaka 146 KK na kuundwa upya na Julius Caesar mwaka 44 KK kama koloni ya Kiroma. Ulikua haraka na kuwa na mchanganyiko wa watu kutoka Italia, Ugiriki na Wayahudi. Wakati Paulo wa Tarso alipofika mwaka 51/52 (taz. Mdo. 18:1-18) alikutana na Aquila na Priscilla na kuunda ushirika wa kikristo pamoja nao. Alirudi tena mwaka 58 akikaa miezi mitatu. Kunauwezekano ya kwamba Waraka kwa Waroma uliandikwa hapa.

Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Korintho kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.