Mtume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtume Paulo.

Mtume, katika maana halisi kama ilivyotolewa kutoka Kigiriki apóstolos, ni "mmoja ambaye ametumwa". Lengo la kutumwa huweza kuwa ni kufikisha ujumbe na hivyo mjumbe ni tafsiri mbadala. Tafsiri nyingine ya kawaida ni pamoja na balozi.

Neno hili hupatikana katika lugha ya Kiyunani ndani ya Agano Jipya na limetumika pale Yesu alipochagua Mitume wake Kumi na wawili (pamoja na Mtume Petro, Mtume Yakobo na Mtume Yohane).

Pia maana ya neno hili inaweza kutumiwa katika miktadha mbalimbali. Mfano hutumika hasa kwa ajili ya washirika wa mapema katika uanzilishi wa dini, ambao walikuwa muhimu katika kueneza mafundisho yake.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.