Nenda kwa yaliyomo

Mtume Yohane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yohane mtume na mwinjili (mchoro wa Simone Martini)
Mitume wa Yesu
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Mtume Yohane (aliishi karne ya 1 B.K.) alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambaye alipendwa na mwalimu wao kuliko wenzake wote.

Pamoja na kaka yake Yakobo na rafiki yao Petro alishuhudia tukio la Yesu Kugeuka sura na la kuteseka katika bustani ya Getsemane, akapokea kutoka kwake Bikira Maria kama mama akiwa chini ya msalaba.

Mapokeo ya Ukristo yanamuona kuwa mwandishi wa Injili ya Yohane, wa barua tatu (Waraka wa kwanza wa Yohane, Waraka wa pili wa Yohane, Waraka wa tatu wa Yohane) na wa Kitabu cha Ufunuo.

Katika maandishi hayo anajitokeza mwanateolojia ambaye, kisha kujaliwa kutazama utukufu wa Neno aliyefanyika mwili, alitangaza aliyoyaona kwa macho yake [1].

Alizaliwa na Zebedayo na Salome baada ya Yakobo mwanzoni mwa karne ya 1 akafa mkongwe mwishoni mwa karne hiyo huko Efeso (katika Uturuki wa leo).

Kabla ya kumfuata Yesu Kristo alikuwa mvuvi na mfuasi wa Yohane Mbatizaji.

Ndiye shahidi mkuu wa miaka mitatu hivi ya utume wa Yesu, akiwa wa kwanza kumfuata (pamoja na Mtume Andrea), mshiriki wa matukio ya pekee ya mwalimu wake (kama alipogeuka sura mlimani), mtume pekee aliyesimama chini ya msalaba, wa kwanza kusadiki ufufuko wa Yesu hata kabla hajamuona.

Kutokana na udhati wa teolojia yake alifananishwa na tai.

Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Desemba[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 467-468
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 404-406
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 96

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtume Yohane kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.