Mtume Mathayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mtume Mathayo
Mitume wa Yesu

Mathayo (kwa Kiebrania מַתִּתְיָהוּ, Mattityahu au מתי, Mattay, Zawadi ya Mungu; kwa Kigiriki Ματθαῖος, Matthaios) ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa kama mtakatifu na Wakristo wengi sana, hasa kutokana na Injili yenye jina lake. Labda aliitwa pia Lawi.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kabla hajaitwa na Yesu Kristo amfuate, Mathayo alikuwa mtozaushuru, na kwa sababu hiyo alitazamwa na Wayahudi msaliti wa taifa na mkosefu. Hata hivyo Yesu alipomkuta forodhani alimuambia, "Nifuate" (Injili ya Marko 2:14). Ndipo Mathayo akaacha vyote akaanza kuwa mwanafunzi wake. Katika nafasi hiyo alimuandalia karamu kubwa waliyoishiriki watozaushuru wengi, hata kusababisha lawama toka kwa Mafarisayo.

Inasemekana kwamba baada ya ufufuko wa Yesu, Mathayo alieneza habari njema Ethiopia, ingawa masalia yake yanaheshimiwa huko Salerno (Italia) tangu mwaka 954.

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Kuna ushahidi wa zamani kwamba aliwahi kuandika misemo ya Yesu kwa lugha ya Kiaramu. Kitabu hicho kilipotea mapema, na ni vigumu kusema kina uhusiano gani na Injili ya Mathayo iliyoandikwa moja kwa moja kwa Kigiriki fasaha.

Heshima baada ya kifo[hariri | hariri chanzo]

Wakristo wa madhehebu yote wanamheshimu kama mtakatifu, hasa tarehe 21 Septemba na 16 Novemba.

Anaheshimiwa kama msimamizi wa watu wa benki, forodha, watunzahesabu n.k.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: