Mtume Mathia
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mtume Matia)
Mitume wa Yesu |
---|
|
Mtume Mathia (kwa Kigiriki Matthias kutokana na Mattathias, kwa Kiebrania Mattithiah, maana yake "Zawadi ya Mungu") kadiri ya Matendo ya Mitume 1:21-22 alikuwa mfuasi wa Yesu Kristo tangu alipobatizwa na Yohane Mbatizaji hadi alipopaa mbinguni mwaka 30 (au 33).
Kabla ya Pentekoste wa mwaka huo, Mtume Petro alipendekeza kwamba mmoja kati ya wafuasi wa kwanza wa Yesu ashike nafasi ya marehemu mtume Yuda Iskarioti, na kura ya bahati ilimuangukia Mathia awe shahidi wa ufufuko wake.
Ingawa Biblia haina habari zaidi juu yake, inasemekana alifia dini na tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 14 Mei (Kanisa Katoliki[1] na Anglikana), tarehe 9 Agosti (Waorthodoksi wa Mashariki) na tarehe 24 Februari (Walutheri na wengineo).
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Mathia kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |