Mtume Mathia
Mandhari
| Mitume wa Yesu |
|---|
|
Mtume Mathia (kwa Kigiriki Matthias kutokana na Mattathias, kwa Kiebrania Mattithiah, maana yake "Zawadi ya Mungu") kadiri ya Matendo ya Mitume 1:21-22 alikuwa mfuasi wa Yesu Kristo tangu alipobatizwa na Yohane Mbatizaji hadi alipopaa mbinguni mwaka 30 (au 33).
Kabla ya Pentekoste wa mwaka huo, Mtume Petro alipendekeza kwamba mmoja kati ya wafuasi wa kwanza wa Yesu ashike nafasi ya marehemu mtume Yuda Iskarioti, na kura ya bahati ilimuangukia Mathia awe shahidi wa ufufuko wake [1].
Ingawa Biblia haina habari zaidi juu yake, inasemekana alifia dini na tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 14 Mei (Kanisa Katoliki[2] na Anglikana), tarehe 9 Agosti (Waorthodoksi wa Mashariki) na tarehe 24 Februari (Walutheri na wengineo).
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 151-153
- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 166-167
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 139-140
- Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 41
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Mathia kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
