Waraka wa kwanza kwa Wathesaloniki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya

Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike ni sehemu ya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Ni barua iliyoandikwa na Paulo wa Tarso kwa Wakristo wa mji wa Thesaloniki katika Ugiriki ya Kale.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Muda wa uandishi[hariri | hariri chanzo]

Barua hiyo ni andiko la kwanza la Agano Jipya katika Biblia kwa kuwa ni wa mwaka 51 hivi.

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Paulo alikuwa amekimbia Thesalonike baada ya wiki 3 tu za utume, hivyo aliogopa kwamba huenda dhuluma zikawakatisha wanafunzi tamaa. Kumbe, akina Timotheo walipofika Korintho toka Thesaloniki, walimpa Mtume Paulo ripoti kuhusu hali ya Kanisa la kule na kumuondolea wasiwasi: dhuluma zilikuwa zikiendelea lakini Wakristo wachanga wa huko ni imara katika imani yao mpya, isipokuwa hawaelewi vizuri mambo fulanifulani, hasa kuhusu vikomo vya binadamu.

Hapo Paulo akawaandikia kwa furaha barua tuliyonayo mpaka leo ili kuwahimiza na kuwaelimisha zaidi: haina mafundisho mazito isipokuwa kuhusu mambo ya mwisho (hali ya marehemu na ujio wa pili wa Bwana).

Ni barua tulivu na ya kirafiki, ingawa inatoa maonyo upande wa maadili (1Thes 1:1-3:13; 4:13-17; 5:1-11; 5:16-28).

Mpangilio[hariri | hariri chanzo]

Mpangilio wa barua ni uleule wa zile zitakazofuata: baada ya salamu na shukrani kwa Mungu, yanafuata mafundisho ya imani, halafu maadili, na hatimaye salamu nyingine.

Kiungo cha nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili

]