Waraka wa Yuda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya


Hiki ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi[hariri | hariri chanzo]

Hatujui vizuri mwandishi ni nani (ingawa anajiita ndugu wa Yakobo), wala aliandika lini (wengi wanakisia miaka ya 80 B.K.), wala aliwaandikia akina nani (barua ni kwa wote, ingawa baadhi wanahisi walengwa kuwa ni Wakristo wa Kiyahudi walio nje ya Israeli).

Mada[hariri | hariri chanzo]

Ujumbe ni kujihadhari na wazushi wanaobunibuni mafundisho mapya badala ya kushika imani ile iliyofunuliwa mara moja na ikatosha; ujumbe huo ulitolewa kwa kuwatukana na kuwalaani wazushi hao (Yuda 1-4, 17-25).


Kiungo cha nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili