Ndui

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mtoto wa Bangladesh aliyepatwa na ndui mwaka 1973.

Ndui (ing. smallpox) ilikuwa ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na aina mbili za virusi: Variola major na Variola minor.

Ulikuwa unaleta kifo cha waliopatwa kwa asilimia 30-35, lakini zaidi kati ya watoto.

Walionusurika wengi waliachwa na makovu ya kudumu hasa katika uso.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Inakadiriwa ulikuwepo miaka 10,000 KK hadi mwaka 1977.

Chanzo chake hakijulikani lakini kuna dalili ya kwamba ilitokea mapema sana katika Misri ya Kale[1]. Kuna dalili ya kwamba farao Ramses V alikuwa mgonjwa wa kwanza anayejulikana kutokana na utafiti wa mumia yake[2]. Labda imepelekwa Uhindini na wafanyabiashara Wamisri mnamo miaka 1500 KK. Ugonjwa uliua watu wengio huko Ulaya[3], Asia na Afrika ilikosambaa pia.

Matokeo ya ndui yalikuwa mabaya hasa huko Amerika ambako Waindio yaani wenyeji asilia waliwahi kuishi milenia nyingi bila mawasiliano na bila maambukizi kutoka sehemu nyingine za dunia hivyo walikosa kabisa kinga. Kwa mfano Wahispania waliweza kuvamia milki ya Azteki huko Mexiko kwa sababu wateteaji wa Tenochtitlan walidhoofishwa na ugionjwa uliopelekwa hapo na Wahispania.

Mwaka 1967 tu ndui iliua watu milioni mbili na katika karne ya 20 kwa jumla milioni 300 au 500.

Ni ugonjwa wa kwanza ambao binadamu kwa njia ya chanjo alifaulu kuukomesha.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Shchelkunov SN (December 2011). "Emergence and reemergence of smallpox: the need for development of a new generation smallpox vaccine". Vaccine. 29 Suppl 4: D49–53. doi:10.1016/j.vaccine.2011.05.037. PMID 22185833.
  2. Hopkins, Donald. "Ramses V:Earliest known victim?" (PDF). WHO imeangaliwa 30-03-2016
  3. J. N. Hays (2005). "Epidemics and pandemics: their impacts on human history". ABC-CLIO. p.151. ISBN 1-85109-658-2
  • Hopkins DR (2002). The Greatest Killer: Smallpox in history. University of Chicago Press. ISBN 0-226-35168-8

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

     . PMID 12496354
      . http://content.nejm.org/cgi/content/full/348/5/460.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: