Homa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kipimajoto ni kifaa cha kupimia homa

Homa ni hali ya mwanadamu kuwa na halijoto ya mwili juu 37 °C. Halijoto ya kawaida ya mwanadamu ni kati ya 36.6 to 37 sentigredi za Selsiasi ikipimwa chini ya ulimi.

Mara nyingi homa husababishwa na ugonjwa; ni dalili ya kwamba kinga cha mwili kinapambana na vijidudu vinavyosababisha ugonjwa fulani.

Homa si ugonjwa mwenyewe bali dalili ya magonjwa mbalimbali. Katika lugha ya kila siku malaria mara nyingi huitwa "homa" ingawa kupanda kwa halijoto ya mwili wakati wa malaria ni dalili ya mapambano dhidi ya vijidudu vya plasmodium tu.

Hadi kiwango cha sentigredi 39 homa si hatari sana lakini kipanda juu ya 40 °C inaanza kudhoofisha maumbile ya mtu hadi kuwa hatari yenyewe. Inashauriwa kumwona daktari na kutumia madawa ya kutuliza homa. Kufikia 42 °C homa inaweza kumwua mtu kwa kusababisha uharibifu wa viungo vya ndani vya mwilini.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]