Miwani
Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama hapa
Miwani ni kifaa cha msaada wa kuona vizuri zaidi kinachotumiwa na watu wenye macho mabovu. Ni kifaa kinachoboresha uwezo wa kuona.
Kwa kawaida miwani ni lenzi mbili za kioo au plastiki zinazoshikwa na fremu. Fremu hulala juu ya pua ikiwa na mikono miwili inayoshikana na masikio.
Aina za lenzi zinateuliwa kutokana na udhaifu wa macho yaani tabia ya lenzi inapaswa kulingana na tatizo la kila jicho.
Kuna pia miwani ya kukinga macho ama dhidi ya jua kali au dhidi ya upepo na vumbi wakati wa kufanya kazi au kwenye burudani ya michezo.
Kundi la madaktari wa ulindaji wa macho American Optometrist Association husema kwamba kila mtu inafaa avae miwani ya sunglasses hasa anapokwenda mahala kuna jua kali ama atajipata akiangalia juu kwenye jua.
Miwani ya nakshi
[hariri | hariri chanzo]Kando ya miwani ya watu walio na udhaifu wa macho, kuna miwani ambayo hutumiwa tu kwa ulibwende na kwa kujitia nakshi. Kwa kawaida miwani hii huvaliwa katika burudani tofauti hasa na vijana.
Historia ya miwani
[hariri | hariri chanzo]Watu wa jamii ya Inuit ndio wakisiwa kuwa wa kwanza kuvalia miwani.
Mmoja wa wafalme wa Dola la Roma, kaisari Nero alikuwa akivalia vilinda macho akiangalia vita.
Katika nchi ya China, miwani ya kwanza ilitengenezwa katika karne ya 12.
Miwani ya kisasa
[hariri | hariri chanzo]Miwani ya kisasa imefanyiwa uvumbuzi mwingi na kutiwa nakshi za kila aina. Lenzi pia zimeweza kuwa za nguvu zaidi na hili linawezesha watu kuona kwa umbali hata wakiwa na udhaifu wa macho.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Miwani kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |