Nenda kwa yaliyomo

Shavkat Mirziyoyev

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shavkat Miromonovich Mirziyoyev (kwa Kiuzbeki: Шавкат Миромонович Мирзиёев; amezaliwa 24 Julai 1957) ni mwanasiasa wa Uzbekistan ambaye amekuwa Rais wa Uzbekistan na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Uzbekistan tangu mwaka 2016. Hapo awali alikuwa Waziri Mkuu wa Uzbekistan kutoka mwaka 2003 hadi 2016.

Kufuatia kifo cha Rais Islam Karimov, aliteuliwa na Bunge Kuu kuwa rais wa mpito wa Uzbekistan mnamo 8 Septemba 2016. Baadaye alichaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa urais wa Desemba 2016, akishinda kwa 88.6% za kura, na aliapishwa mnamo 14 Desemba 2016.

Mnamo Oktoba 2021, Shavkat Mirziyoyev alichaguliwa tena kuwa Rais wa Uzbekistan.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shavkat Mirziyoyev kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.