Wakazakhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wakazakhi (kwa Kikazakhi Қазақ/Qazaq, wingi Қазақтар/Qazaqtar) ni taifa lenye kutumia Kikazakhi, mojawapo ya lugha za Kiturki linalopatikana hasa nchini Kazakhstan, lakini pia katika Mongolia, China, Urusi, Uzbekistan na Afghanistan. Vikundi vidogo zaidi vinapatikana Iran na Uturuki.

Idadi ya Wakazakhi hukadiriwa kuwa mnamo milioni 20.

Upande wa dini walio wengi ni Waislamu Wasunni.

Wakazakhi wametokea katika historia ya makabila ya Kiturki katika Asia ya Kati. Jina "Kazakh" linamaanisha "huru, asiyetawaliwa": lilikuwa namna ya kutaja makabila ya Waturki waliopendelea kufuata mila zao na kujitenga mnamo 1450 na milki ya Wauzbeki.

Maeneo makubwa walipoishi Wakazakhi yalitwaliwa na Urusi kuanzia karne ya 17 kwa hiyo Wakazakhi wengi waliishi katika Milki ya Urusi na katika karne ya 20 katika Umoja wa Kisovyeti.

Baada ya mapinduzi ya kikomunisti Wakazakhi walipewa eneo lao la pekee ndani ya mfumo wa ukomunisti na tangu mwaka 1936 eneo hili lilikuwa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi, moja kati ya jamhuri 17 zilizounda Umoja wa Kisovyeti. Hiyo ilipata uhuru wake tangu kuporomoka kwa ukomunisti mwaka 1991.

Leo hii wanaishi

  1. Kazakhstan 12,212,645 (2018)[1]
  2. China 1,800,000[2]
  3. Uzbekistan 800,000[3]
  4. Urusi 647,732[4]
  5. Mongolia 201,526[5]
  6. Kyrgyzstan 33,200[6]
  7. Marekani 24,636
  8. Uturuki 10,000
  9. Iran 3,000–15,000

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Этнодемографический сборник Республики Казахстан 2014. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-11-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-20.
  2. [The Kazak Ethnic Group (China)]
  3. CIA kuhusu Uzbekistan, inakadiria asilimia 3 za wakazi wote. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-07-09. Iliwekwa mnamo 2019-03-20.
  4. Russia National Census 2010. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-12-23. Iliwekwa mnamo 2019-03-20.
  5. Mongolia National Census 2010 Provision Results. National Statistical Office of Mongolia Archived 15 September 2011 at the Wayback Machine (in Mongolian.)
  6. National Statistical Committee of Kyrgyzstan. National Census 2009 Archived 8 March 2012 at the Wayback Machine. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-20.