Bahari ya Kaspi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bahari Kaspi)
Jump to navigation Jump to search
Caspian Sea
Stenka Razin (Vasily Surikov)

Bahari ya Kaspi (pia Bahari ya Qazwin- Kiajemi دريا خزر "darya khazar"; Kirusi Каспийское море "kaspiiskoye more") ni ziwa kubwa kabisa duniani lenye eno la 371,000 km² na mjao wa 78,200 km³. Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan na Uajemi.

Kimo chake mkubwa ni 1,025 m. Huitwa "bahari" kwa sababu maji yake ni ya chumvi ingawa si kali sana kama ya bahari yenyewe.

Maji ya chumvi[hariri | hariri chanzo]

Upande wa kaskazini inaingia mito miwili mikubwa ya Volga na Ural. Inasababisha kiasi kidogo cha chumvi upande huo wa kaskazini. Asilimia ya chumvi huonegezeka kuelekea kusini.

Madini[hariri | hariri chanzo]

Chini ya bahari kuna akiba kubwa za mafuta ya petroli na gesi hasa karibu na Baku. Katika hori ya Kara-Bogas chumvi hulimwa.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]