Bahari ya Kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bahari ya Kuini inayozunguka bara la Antaktiki
Ramani hii inaonyesha mabadiliko ya halijoto ya maji ya bahari za dunia katika mwendo wa mwaka. Inaonekana jinsi gani kanda la barafu linalozunguka pwani la Antaktika (chini kabisa, rangi ya kijivu) hupanuka na kurudi nyuma kila mwaka

Bahari ya Kusini (pia: Bahari ya Antaktiki) ni jina jipya katika jiografia. Linamaanisha maji yote kusini ya latitudo ya 60 yanayozunguka bara la Antaktiki.

Katika eneo hili maji ya Bahari ya Atlantiki, Bahari Hindi na Pasifiki hukutana na kuingiliana. Kwa muda mrefu wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Hidrografia walihesabu eneo kama vitengo vya kusini vya bahari tatu kubwa lakini katika karne ya 20 wazo la kuitazama kama bahari ya pekee imesambaa na Bahari ya Kusini imerudi kwenye ramani. [1]

Eneo lote ni kilomita za mraba 20,327,000 za maji. Linazunguka pwani la Antaktika lenye urefu wa kilomita 17,968 km. Kina kikubwa ni mnamo 5,805 mita.

Sehemu zake karibu na pwani hufunikwa na barafu inayokua wakati wa baridi. Katika miezi ya joto vipande vikubwa vya barafu huvunjika na kuelea katika maji kama siwa barafu ambako ni hatari kwa ajili ya meli lakini zinayeyuka polepüole kadri jinsi zinavyofika maji yasiyo baridi tena.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Taarifa ya IHO ya 1937 ilifuta jina la Bahari ya Kusini, lakini katika nakala ya 2002, mlango wa 10 imerudishwa.
Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Kusini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.