Shirika la Kimataifa la Hidrografia
Shirika la Kimataifa la Hidrografia (ing. International Hydrographic Organization - IHO) ni taasisi ya kimataifa inayolenga kuunganisha juhudi za kitaifa katika fani ya hidrografia kwa kusudi la kuboresha hasa usalama wa usafiri kwa maji.
Shirika hili lilianzishwa mwaka 1921 na mataifa 19 kwa jina la "International Hydrographic Bureau" (Ofisi ya Kimataifa ya Hidrolojia). Makao makuu yamepelekwa Monaco. Tangu 1970 iko jina la sasa.
Shirika la IHO linasimamia upimaji wa bahari, maziwa na mito yanayotumiwa kwa usafiri wa kimataifa na usanifishaji wa ramani zinazoonyesha kimo cha maji, vizuizi au hatari kwa usafiri kwa maji.
Shirika linatambuliwa na Umoja wa Mataifa kama mshauri mkuu katika mambo yote ya hidrografia.
Mwaka 2006 kulikuwa na mataifa 74 wanachama. Wawakilishi hukutana kila baada ya miaka mitano huko Monaco.