Nenda kwa yaliyomo

Siwa barafu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Siwa barafu
Siwa barafu inaweza kuwa na umbo kama hili; asilimia kubwa iko chini ya maji

Siwa barafu (kwa Kiingereza iceberg) ni pande kubwa la barafu linaloelea baharini. Siwa barafu inaweza kusukumwa na mikondo ya baharini hadi kufika kwenye maji vuguvugu inapoyeyuka; kinyume chake inaweza kusukumwa dhidi ya maganda makubwa ya barafu na kuunganika nayo.

Asili ya siwa barafu

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida siwa barafu hupatikana kama pande la barafuto lilomegeka linaloishia pwani na kutumbukia kwenye maji ya bahari. Njia nyingine ni kuvunjika kwa vipande vya maganda ya barafu yanayofunika [[ncha ya kaskazini ya dunia]] na Antaktika.

Barafu ni nyepesi kushinda maji na hivyo kipande cha barafu kitaelea kwenye maji lakini sehemu kubwa ya siwa barafu iko ndani ya maji.

Siwa barafu huelea pamoja na mwendo wa mikondo ya bahari. Kadiri inavyofika kwenye maji yasiyo baridi tena, muda wa maisha ni miezi hadi miaka kadhaa. Muda huo hadi kuyeyuka kabisa unategemea ukubwa wa siwa barafu na halijoto ya eneo inapofikia. Zimetazamwa kwa muda wa miaka 3.

Mara nyingi zinaonekana mita 1 hadi 75 juu ya uso wa bahari; uzito hufikia hadi tani 100,000 au 200,000. Siwa barafu kubwa katika Atlantiki ya kaskazini iliyotazamwa ilikuwa na mita 168 juu ya maji yaani kimo cha nyumba ya ghorofa 55.

Siwa barafu kubwa iliyopimwa hadi sasa ilikuwa pande kubwa lililomeguka Antaktika mwaka 2000; urefu wake ulikuwa kilomita 295 na upana kilomita 37. Eneo lake lilikuwa km² 11,000 na masi yake tani bilioni tatu.

Hatari kwa meli

[hariri | hariri chanzo]

Siwa barafu ni hatari kwa meli kwa sababu sehemu kubwa iko ndani ya maji; asilimia 10 pekee inaonekana juu ya uso wa bahari. Kama meli inakaribia mno kuna uwezekano ya kwamba siwa barafu iko ndani ya maji mita mamia kutoka kilele chake kinachoonekana juu, na meli inaweza kugonga sehemu ile isiyoonekana.

Kwa njia hiyo ajali zinatokea tena na tena na mfano mashuhuri ni ajali ya meli Titanic iliyozama chini mwaka 1912 baada ya kugongana na siwa barafu. Watu zaidi ya 1,500 walikufa baharini.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siwa barafu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.