Ghuba ya Kalifornia
Ghuba ya California (pia: Bahari ya Cortez, inajulikana kwa lugha ya Kihispania kama Mar de Cortes au Golfo de California. kwa Kiingereza: Gulf of California) ni sehemu ya bahari iliyopo kati ya rasi ya Baja California na Meksiko bara. Eneo lake ni kama km² 160,000.
Jina na mipaka
[hariri | hariri chanzo]Imepakana na majimbo ya Baja California, Baja California Sur, Sonora, na Sinaloa.
Kwenye ramani za kimataifa huitwa zaidi "Ghuba ya Kalifornia". Watu wa maeneo jirani hupendelea jina "Bahari ya Cortes" kwa kumbukumbu ya Hernando Cortes, mtekaji Mhispania wa Mexiko.
Jiolojia
[hariri | hariri chanzo]Ghuba ya California ilitokea miaka milioni 5.3 iliyopita kutokana na miendo katika ganda la Dunia iliyoitenga na bamba la Amerika ya Kaskazini na kufanywa kama sehemu za uso wa sayari zilipohamisha Hifadhi ya Baja California mbali na Bamba la Amerika Kaskazini.
Volkeno zilitokea katika mchakato huo na kisiwa cha Isla Tortuga ni mfano mmojawapo wa volkano zinazopatikana. [1]
Visiwa
[hariri | hariri chanzo]Ndani ya ghuba kuna visiwa viwili vikubwa, Isla Ángel de la Guarda na Kisiwa cha Tiburon, pamoja na visiwa vingine vidogo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Science Plans RCL". review.nsf-margins.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-18. Iliwekwa mnamo 2008-05-27.
Tovuti za Nje
[hariri | hariri chanzo]- Sea of Cortez Expedition and Education Project Ilihifadhiwa 20 Julai 2009 kwenye Wayback Machine.
- Jumba la Desert Museum
- CEDO Intercultural Ilihifadhiwa 3 Novemba 2015 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ghuba ya Kalifornia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |