Bahari ya Solomon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bahari ya Solomon

Bahari ya Solomon ni sehemu ya Bahari Pasifiki iliyopo kati ya Papua Guinea Mpya na Visiwa vya Solomon.

Bahari ya Solomon inajumuisha mfereji wa New Britain unaofikia kina cha zaidi ya mita 9,140 chini ya usawa wa bahari. [1]

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia yalitokea mapigano mengi katika sehemu hiyo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Solomon Sea. Encyclopaedia Britannica. Iliwekwa mnamo 10 March 2012.