Nenda kwa yaliyomo

Bahari ya Okhotsk

Majiranukta: 55°N 150°E / 55°N 150°E / 55; 150
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

55°N 150°E / 55°N 150°E / 55; 150

Ramani ya Bahari ya Okhotsk.

Bahari ya Okhotsk ni bahari ya pembeni ya Pasifiki ya magharibi. [1] Iko kati ya rasi ya Kamchatka upande wa mashariki, visiwa vya Kurili upande wa kusini mashariki, kisiwa cha Hokkaidō upande wa kusini, kisiwa cha Sakhalin kwenye magharibi, na pwani ya Siberia ya mashariki upande wa magharibi na kaskazini. Ghuba ya Shelikhov iko upande wa kaskazini mashariki.

Jina limetokana na mji wa Okhotsk ambayo ni mji wa kwanza ulioundwa na Warusi katika Mashariki ya Mbali.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi ya taifa ya Shiretoko kwenye pwani ya Hokkaido, Japan.
Ramani inaonyesha kina cha maji katika Bahari ya Okhotsk.

Eneo la Bahari ya Okhotsk ni km2 1,583,000. Imeunganishwa na Bahari ya Japani upande wa magharibi kupitia Ghuba ya Sakhalin, upande wa kusini kupitia mlangobahari wa La Pérouse. Kina cha wastani ni mita 859, kina kirefu zaidi ni mita 3,372.

Katika majira ya baridi, usafiri kwenye Bahari ya Okhotsk unakuwa mgumu, au hata hauwezekani, kwa sababu ya wingi wa barafu.

Visiwa[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya visiwa vya Bahari ya Okhotsk ni vikubwa kiasi. Hii ni pamoja na Hokkaido ambayo ni kisiwa cha pili kwa ukubwa cha Japani, na Sakhalin ambayo ni kisiwa kikubwa cha Urusi. Visiwa vingi vidogo vya bahari hiyo havina wakazi, hivyo ni maeneo bora ya kuzaliana kwa sili na pinnipedia wa spishi mbalimbali pamoja na ndege wa baharini.

Bandari za maana[hariri | hariri chanzo]

Hori ya Nagayevo karibu na Magadan, Urusi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kon-Kee Liu; Larry Atkinson (Juni 2009). Carbon and Nutrient Fluxes in Continental Margins: A Global Synthesis. Springer. ku. 331–333. ISBN 978-3-540-92734-1. Iliwekwa mnamo 29 Novemba 2010.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Tovuti za Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Okhotsk kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.