Bahari ya Greenland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la Bahari ya Greenland

Bahari ya Greenland ni jina la sehemu ya Bahari Aktiki iliyopo upande wa mashariki wa Greenland.

Inapakana na kisiwa cha Greenland upande wa magharibi, funguvisiwa la Svalbard upande wa mashariki, na Bahari ya Norwei pamoja na Iceland upande wa kusini. Upande wa kaskazini ziko sehemu za Bahari Aktiki zinazofunikwa kwa barafu kwa miezi mingi ya mwaka. [1][2][3].

Eneo lake ni mnamo kilomita za mraba 1,205,000. Kina cha wastani ni mita 1,444, kina kikubwa ni mita 4,846.

Tabianchi ni baridi sana; halijoto hupanda kwa muda mfupi tu juu ya °C 0. Baridi iliyopimwa ilikuwa °C -49 karibu na Spitsbergen, lakini kisiwani Greenland joto limeshafikia °C +25 kwa muda mfupi. Wastani ni baina ya °C -10 (kusini) hadi - 26 (kaskazini) wakati wa February na baina ya °C +5 hadi 0 wakati wa Agosti.

Hata hivyo maji ya bahari hujaa uhai wa samaki na wanyama kama sili na nyangumi wanaovindwa na Waeskimo waliokalia pwani za Greenland kwa karne nyingi.

Visiwa vikubwa ni pamoja na funguvusiwa la Svalbard, Kisiwa cha Edvards, Eila, Godfred Hansens, Ile-de-France, Jan Mayen na mengine, Kisiwa cha Spitsbergen katika Svalbard pekee ina wakazi wa kudumu[4].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Greenland Sea (Russian). Great Soviet Encyclopedia. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-12-25. Iliwekwa mnamo 2019-09-17.
  2. Greenland Sea. Encyclopædia Britannica on-line.
  3. Greenland Sea, MarBEF Data System - European Marine Gazetteer
  4. Islands of Greenland (Denmark) Archived 19 Aprili 2016 at the Wayback Machine., United Nations Environment Programme (UNEP)