Bahari ya Sargasso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Coordinates: 28°N 66°W / 28°N 66°W / 28; -66

Bahari ya Sargasso.
Mwani wa sargassum unafunika maeneo makubwa ya bahari

Bahari ya Sargasso ni eneo la Bahari Atlantiki lililoko upande wa mashariki wa Florida.

Hakuna pwani za nchi kavu[1] lakini hutajwa kama eneo la pekee kwa sababu linazungukwa na mikondo ya bahari yenye mwendo wa kiduara[2].

Mwendo wa mikondo kwenye mipaka yake husababisha sehemu za uso wa Bahari ya Saragasso kuwa chini ya usawa wa bahari ya jirani na hivyo mwani unaoelea kwenye maji hukusanyika huko. [3] Kwa jumla maji ya sehemu hii ni safi sana bila machafuko inayomaanisha kibiolojia kuna lishe kidogo kwa uhai ndano yake. Lakini kuna mwani wa sargassum unaoelea kwenye uso wa maji na kuwa mazingira yanayoyoruhusu spishi mbalimbali kustwi hapa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sea. National Geographic Society (27 September 2011). Iliwekwa mnamo 27 June 2017. “...a sea is a division of the ocean that is enclosed or partly enclosed by land...”
  2. (2004) Encyclopedia of the Oceans. Oxford University Press, 90. ISBN 978-0198606871. Retrieved on 27 June 2017. 
  3. NOS Staff (25 March 2014). What's the Difference between an Ocean and a Sea?. Ocean Facts. National Ocean Service (NOS), National Oceanic and Atmospheric Administration (NOAA).

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: