Nenda kwa yaliyomo

Bahari ya Celebes

Majiranukta: 3°N 122°E / 3°N 122°E / 3; 122
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bahari ya Sulawesi)
Mazingira ya Bahari ya Celebes.
Bahari ya Celebes.
Pwani kwenye Bahari ya Celebes.

Bahari ya Celebes (kwa Kiingereza: Celebes Sea) au Bahari ya Sulawesi (kwa Kiindonesia: Laut Sulawesi) ni sehemu ya Bahari Pasifiki ya magharibi.

Inapakana na visiwa vya Sulawesi (pia Celebes, nchini Indonesia) upande wa kusini, Borneo yenye jimbo la Kalimantan (Indonesia) na Sabah (Malaysia) upande wa magharibi na Mindanao (Ufilipino) upande wa kaskazini. Upande wa mashariki viko visiwa vya Sangihe.

Mbali na visiwa kuna Bahari kubwa ya Pasifiki upande wa mashariki na Bahari ya Ufilipino upande wa kaskazini.

Eneo lake ni mnamo kilomita za mraba 280,000, upana wake ni kilomita 675 kutoka kaskazini hadi kusini, na urefu wake ni km 837 kutoka magharibi hadi mashariki. Kina cha maji huwa na urefu wa mita 6,200.

Ekolojia

[hariri | hariri chanzo]
Ngisi wa jenasi Enoploteuthis hutoka Bahari ya Celebes

Bahari ya Celebes ina maji vuguvugu na safi. Kuna spishi nyingi zinazopatikana huko kama vile nyangumi, pomboo, kasa, taa, mizira na jodari. Miwani huvunwa pia. Upande wa matumbawe spishi 580 kati ya 793 zinazojenga miamba zimeonekana huko.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

3°N 122°E / 3°N 122°E / 3; 122

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Celebes kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.