Mfereji wa Msumbiji
Mandhari
Mfereji wa Msumbiji (kwa Kiingereza Mozambique Channel, kwa Kifaransa Canal du Mozambique, kwa Kimalagasi: Lakandranon'i Mozambika, kwa Kireno: Canal de Moçambique) ni sehemu ya Bahari Hindi iliyopo kati ya kisiwa cha Madagaska na bara la Afrika, hasa nchi ya Msumbiji.
Sehemu yake nyembamba yenye upana wa kilomita 460 iko kati ya Angoche, Msumbiji na Tambohorano, Madagaska. Urefu wake ni takribani km 1,600. Maji yake yanafikia kina cha mita 3,292 .
Mfereji huu unapitiwa na mkondo wa bahari unaopeleka maji ya vuguvugu hadi pwani ya Afrika Kusini.