Nenda kwa yaliyomo

Îles Éparses

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Iles Eparses)
Ramani ya Îles éparses

Îles éparses (Kifaransa kwa "visiwa vilivyotawanyika") ni atolli na visiwa vidogo katika Bahari Hindi vinavyotawaliwa na Ufaransa. Haviko chini ya mkoa wowote au kitengo kingine kati ya maeneo ya ng'ambo ya Ufaransa. Havihesabiwi kama mkoa wa pekee kwa sababu hakuna wakazi asilia isipokuwa watumishi wa serikali, wanajeshi au wanasayansi kwenye vituo mbalimbali visiwani.

Hadi 2005 vilisimamiwa na mkuu wa mkoa wa Reunion lakini havikuhesabiwa kati ya maeneo ya Umoja wa Ulaya kama Reunion yenyewe. Tangu 2005 kuna afisa mtawala mwenye cheo cha mkuu wa mkoa (prefect) kwa ajili ya isles esparsees pamoja na visiwa katika Bahari ya Antaktika.

Visiwa hivi hudaiwa pia na Madagaska na Tromelin inadaiwa na Shelisheli.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]