Nenda kwa yaliyomo

Ngazija

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Ngazija
Ramani ya Ngazija (Grande Comore)
Mahali pa Ngazija kati ya Msumbiji na Madagaska

Ngazija au Grande Comore (Kifaransa: "Komori Kuu") ni kisiwa kikubwa cha funguvisiwa ya Komori ambayo ni nchi ya visiwani katika Bahari Hindi. Ngazija ni jimbo la kujitawala lenye rais na serikali yake katika shirikisho la Komori.

Eneo la kisiwa ni 1012.9 km². Umbali wake na pwani la Afrika bara ni kilomita 400 hadi Msumbiji. Kijiolojia ni kisiwa changa kushinda visiwa vingine vya Komori. Mlima mkubwa ni volkeno hai ya mlima Karthala mwenye kina cha 2361 m juu ya UB. Eneo kubwa kwenye kaskazini halifai kwa kilimi kwa sababu ni mawemawe tu bila maji.

Kwenye mitelemko ya tako la kisiwa chini ya bahari kuna samaki za pekee za gombessa (jenasi latimeria) zinazotazamiwa kuwa kiungo kati ya samaki na wanyama wa nchi kavu.

Kuna takriban wakazi lakhi tatu na nusu. Mji mkuu ni Moroni ambao ni pia mji mkuu wa kitaifa.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ngazija kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.