Bahari ya Barents

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Bahari ya Barents.

Bahari ya Barents (Kinorwei: Barentshavet; Kirusi: Баренцево море Barentsevo More) ni tawi la Bahari ya Aktiki, na iko kaskazini kwa Urusi, Norwei na funguvisiwa la Svalbard pamoja na Kisiwa cha Dubu. Visiwa vya Novaya Zemlya vinaitenganisha na Bahari ya Kara.

Eneo lake ni la km² 1,424,000. Jina limetokana na baharia Mholanzi Willem Barents.

Sehemu hii ya bahari haina kina kirefu, kwa wastani ni mita 230 pekee. Kiuchumi ni muhimu kwa uvuvi na uchumbaji wa gesi na mafuta ya petroli.

Hata kama ni sehemu ya Bahari ya Aktiki, inaweza kupitiwa na meli karibu mwaka wote kwa sababu inapokea maji ya vuguvugu kutoka Mkondo wa Ghuba wa Bahari Atlantiki unaoishia hapa. Maji ya vuguvugu ni msingi kwa kuota kwa planktoni ambayo ni lishe kwa aina nyingi za samaki.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.