Bahari ya Kiarabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bahari ya Uarabuni)
Bahari ya Kiarabu
ramani ya Bahari ya Kiarabu

Bahari ya Kiarabu (kwa Kiarabu: بحر العرب bahr al-arab) ni sehemu ya kaskazini ya Bahari Hindi iliyopo baina ya Bara Arabu na Bara Hindi. Eneo lake ni takribani kilomita za mraba 4,82,000 ilhali kina kirefu ni mita 4,652.[1].

Upande wa kaskazini inapakana na Pakistan na Iran, upande wa magharibi na Omani, Yemen na Somalia, upande wa mashariki na Uhindi. Ghuba ya Aden iko upande wa magharibi-kusini na hapa mlangobahari wa Bab el Mandeb ni njia ya kuingia Bahari ya Shamu. Ghuba ya Oman inaunganisha na Ghuba ya Uajemi.

Mpaka wa kusini ni mstari baina ya rasi ya Bara Hindi hadi Rasi Guardafui kwenye Pembe la Afrika.

Mto mkubwa unaoishia humu ni mto Indus.

Visiwa si vingi, ni pamoja na Sokotra (Yemen), Masirah (Omani), Lakshadweep (Uhindi) na Astola (Pakistan).

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Arabian Sea, tovuti ya britannica.com, iliangaliwa 13-09-2019

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Kiarabu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.