Nenda kwa yaliyomo

Bahari ya Matumbawe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mazingira ya Bahari ya Matumbawe
Bahari ya Matumbawe

Bahari ya Matumbawe (kwa Kiingereza: Coral Sea; kwa Kifaransa: Mer de Corail) ni sehemu ya Bahari Pasifiki mbele ya pwani ya kaskazini-mashariki ya Australia.

Inapakana na Australia, Papua Guinea Mpya, Visiwa vya Solomon na Kaledonia Mpya.

Tabianchi ni ya joto, usimbishaji ni kati ya milimita za mvua 1,000 hadi 3,000 kwa mwaka, sehemu kubwa hunyesha baina ya Desemba na Machi. Siku za Jua kuonekana ni kati ya 80 hadi 125 kwa mwaka, jotoridi hucheza kati ya sentigredi 18–27°C.

Sehemu hii ya bahari huwa imejaa visiwa vidogo na miamba tumbawe ambayo ndiyo asili ya jina lake. Mkusanyiko mkubwa zaidi wa miamba tumbawe ni Great Barrier Reef mbele ya pwani ya Australia.

Makala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Matumbawe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.