Great Barrier Reef

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Great Barrier Reef jinsi inavyoonekana kutoka angani; kaskazini iko upande wa kulia

Great Barrier Reef ni jina la kimataifa la safu ndefu ya miamba tumbawe inayokaa katika Bahari ya Matumbawe mbele ya pwani ya Australia kwa urefu wa kilomita 2,600.

Ni safu ya mwamba tumbawe kubwa kabisa duniani ikiwa na miamba tumbawe 2,900 ya pekee na visiwa 900 katika eneo la km² 344,400. Safu hii ya mwamba tumbawe inaonekana kutoka anga-nje upande wa mashariki-kaskazini wa Australia mbele ya pwani ya Queensland.

UNEP imeiita moja kati ya maajabu saba asilia za dunia na imepokewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Ni mahali muhimu kwa ekolojia ya bahari; ina aina 359 za matumbawe magumu na aina 80 za matumbawe laini, aina za sifongo 1,500 pia aina za samaki 1,500 pamoja na viumbe vingine vingi.

Great Barrier Reef inavuta watalii wengi Australia kutoka pande zote za dunia zinazovutwa na maajabu ya dunia hii chini ya maji.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.