Mwamba tumbawe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Miamba tumbawe)

Mwamba tumbawe (pia: fufuwele, chawe) ni mawe laini yanayopatikana chini ya bahari, au kando ya bahari.

Miamba tumbawe hujengwa na wanyama wadogo wanaoitwa matumbawe. Aina nyingi za matumbawe hujijengea kiunzi nje; wakati tumbawe anakufa wengine huendelea kujenga nafasi zao juu ya watangulizi na kwa njia hii kukuza miamba tumbawe na hata visiwa vikubwa.

Miamba hiyo ni muhimu katika bahari kwa sababu inatumiwa na samaki kwa mazalia. Miamba hii iko hatarini kupotea.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwamba tumbawe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.