Bahari ya Labrador

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Bahari ya Labrador
Nyangumi na siwa barafu katika Bahari ya Labrador

Bahari ya Labrador (kwa Kiingereza: Labrador Sea, kwa Kifaransa: mer du Labrador) ni mkono wa Bahari Atlantiki uliopo baina ya rasi ya Labrador na Greenland. Upande wa kaskazini unaendelea katika Hori ya Baffin kupitia Mlangobahari wa Davis.[1] Imeitwa pia bahari ya pembeni (en:marginal sea ya Atlantiki.[2][3]

Kina cha Bahari ya Labrador kinafikia mita 3400 kwenye kusini inapounganishwa na Atlantiki; katika sehemu hii ina upana wa km 1,000. Upande wa kaskazini kina hupungua hadi mita 700 ikipita kwenye mlangobahari wa Davis.[4]

Halijoto ya maji haipandi juu ya sentigredi 5-6 na wakati wa baridi theluthi mbili za uso wake zinaganda kuwa barafu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Coordinates: 61°N 56°W / 61°N 56°W / 61; -56 (Labrador Sea)