Bahari ya Laptev

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bahari ya Laptev

Bahari ya Laptev ni bahari ya pembeni ya Bahari ya Aktiki kaskazini kwa Urusi. Iko kati ya pwani la kaskazini ya Siberia, rasi ya Taimyr, Severnaya Zemlya na Visiwa vya Siberia Mpya. Eneo la 672.000 км²

Iko katikati ya Bahari ya Kara kwenye magharibi na Bahari ya Mashariki ya Siberia.

Mto Lena ni mto mkubwa unaoishia hapa katika delta pana.

Tabianchi ni baridi sana. Kutokana na latitudo karibu na ncha ya kaskazini usiku wa majirabaridi na mchana wa majirajoto hudumu miezi kadhaa.

Halijoto ya hewa iko chini ya sentigredi 0 kwa miezi 11 kila mwaka. Sehemu kubwa ya mwaka bahari imefunikwa na ngao ya barafu inayoweza kukua hadi unene wa mita 20-25.

WikiLettreMini.svg Makala hii kuhusu "Bahari ya Laptev" ni fupi mno. Inahitaji kupanuliwa mapema.