Nenda kwa yaliyomo

Ghuba ya Meksiko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Ghuba ya Meksiko ionyeshayo kimo cha milima na kina cha bahari
Mtambo wa mafuta ya petroli katika maji ya Ghuba ya Meksiko

Ghuba ya Meksiko ni hori kubwa au bahari ya pembeni ya Atlantiki inayozungukwa pande tatu na nchi kavu ya Amerika Kaskazini. Kina cha maji hufikia hadi mita 4,375.

Pwani ya ghuba linapakana na nchi zifuatazo:

Mlango wa bahari wa Florida Straits (kati ya Marekani na Kuba) unafungua njia kwenda Atlantiki na mfereji wa Yucatan (kati ya Meksiko na Kuba) unaiunganisha ghuba na Bahari ya Karibi verbunden.

Ghuba yote ina eneo la takriban 1,600,000 km². Maji yake ni ya halijoto ya vuguvugu hata juu ya 26 °C wakati wa miezi ya joto. Hali hii husababisha kutokea kwa dhoruba na tufani za mara kwa mara zinazoleta uharibifu mwingi kwenye visiwa na nchi kavu ya jirani.

Ghuba ya Meksiko ni asili ya mkondo mkubwa wa maji ya vuguvugu unaoelekea kaskazini hadi Ulaya unaojulikana kama mkondo wa Ghuba. Mkondo huu ni msingi kwa hali ya hewa ya Ulaya.

Msingi wa bara chini ya bahari ni mpana. Kuna akiba za mafuta ya petroli ndani yake zinazovutwa na mitambo mingi inayosimama katika maji yenye kina kidogo cha msingi wa bara.