Tamaulipas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bonde la Marcela,Sierra Peña Navada, Sierra Peña Navada,
Bendera ya Tamaulipas
Mahali pa Tamaulipas katika Mexiko

Tamaulipas ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kaskazini-mashariki ya nchi. Upande wa mashariki ni maji ya Ghuba ya Meksiko.

Mji mkuu ni Ciudad Victoria na mji mkubwa ni Reynosa. Imepakana na Marekani (Texas), Veracruz, San Luis Potosí na Nuevo León.

Jimbo lina wakazi wapatao 3,024,238 (2005) wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 79,384.

Gavana wa jimbo ni Eugenio Hernández Flores.

Lugha rasmi ni Kihispania.

Miji Mkubwa[hariri | hariri chanzo]

  1. Reynosa (507,998)
  2. Matamoros (422,711)
  3. Tampico (303,635)
  4. Nuevo Laredo (348,387)
  5. Ciudad Victoria (278,455)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tamaulipas kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.