Nenda kwa yaliyomo

Kigeorgia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kigeorgia (jina la wenyewe: ქართული ენა - kartuli ena) ni lugha rasmi nchini Georgia inazungumzwa na takriban watu milioni 4.5 - 5.

Ni moja kati ya lugha za Kaukazi za Kusini yenye alfabeti yake ya pekee yenye herufi 33 pamoja na 5 nyingine zisizotumika sana.

Lugha ni ya kale, ila imepokea maneno mengi kutoka Kigiriki, Kilatini, Kiajemi, Kiarabu, Kirusi, Kituruki na Kiingereza. Ilianza kuandikwa baada ya Wageorgia kupokea Ukristo katika karne ya 4 BK.

Nje ya nchi ya Georgia lugha hii au lahaja za karibu zinatunmika katika nchi jirani za Kaukazi, Urusi, Uturuki na Israeli walipohamia Wayhudi Wageorgia wengi.

Majina mengi ya Kigeorgia yanaishia kwa -dze ("mwana") (Georgia ya magharibi) au -shvili ("mtoto") (Georgia ya mashariki). Mifano mashuhuri ya watu wanaojulikana kimataifa ni Josef Stalin (dikteta wa Umoja wa Kisovyeti hadi 1953) na Eduard Shevardnadze (waziri wa mambo ya nje wa mwisho wa Umoja wa Kisovyeti na raisi wa Georgia hadi 2003).

Kigeorgia ina maneno mengi yanayoanza kwa konsonanti mbili, tatu au zaidi kwa mfano:

  • წყალი (ts'q'ali), "maji"
  • სწორი, (sts'ori), "sahihi"
  • რძე , (rdze), "maziwa"
  • თმა, (tma), "nywele"
  • მთა, (mta), "mlima"
  • ცხენი, (tskheni), "farasi"
 • Kuna maneno mengi yanayoanza kwa konsonanti 3:
  • თქვენ, (tkven), "ninyi"
  • მწვანე, (mts'vane), "kibichi"
  • ცხვირი, (tskhviri), "pua"
  • ტკბილი, (t'k'bili), "tamu"
  • ჩრდილოეთი, (črdiloeti), "kaskazini"
 • Maneno machache huanza kwa konsonanti 4:
  • მკვლელი, (mk'vleli), "mwuaji"
  • მთვრალი, (mtvrali), "mlevi"
 • Neno hili laanza kwa konsonanti 6:
  • მწვრთნელი, (mts'vrtneli), "mwalimu wa michezo"
 • neno hili linaanza kwa konsonanti 8:
  • გვბრდღვნი (gvbrdgvni), "mnatuvuta"

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]