Nenda kwa yaliyomo

Kilatini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Latin)
Kilatini
Lingua Latina (la)
Lugha
Asili Italia (Dola la Roma)
Wasemaji

L1 : Hakuna wasemaji wa asili
L2: Takriban milioni moja (wasemaji wa Kilatini cha kisasa)

Jumla: ~1 milioni
Familia za lugha Kihindi-Kiulaya
Kilatini-Kihispania
Kilatini-Faliski
Aina za Awali Kihindi-Kiulaya cha Kale
Kilatini cha Kale
Kilatini cha Kawaida
Mfumo wa kuandika Alfabeti ya Kilatini
Lugha Rasmi
Lugha rasmi kwa Mji wa Vatikani
Nambari za Msimbo
ISO 639-1 la
ISO 639-2 lat
Glottolog lati1261
Nahau ya Kilatini ("Kukosa ni jambo la kibinadamu").

Kilatini (Lingua Latina la) ni lugha ya kale ya Kihindi-Kiulaya ambayo ilizungumzwa katika Dola la Roma. Ilianza kama lugha ya eneo la Lazio nchini Italia na baadaye ikawa lugha kuu ya utawala wa Kirumi, ikienea kote Ulaya kupitia upanuzi wa Dola la Roma. Ingawa haizungumzwi tena kama lugha ya asili, Kilatini bado hutumika katika taasisi za kidini, sayansi, sheria, na elimu ya juu, hasa katika Mji wa Vatikani na taasisi za kitaaluma. Lugha za Kirumi kama Kihispania, Kifaransa, Kiitaliano, Kireno, na Kiromania zilichipuka kutoka Kilatini cha Kawaida (Vulgar Latin), ambacho kilitumiwa na watu wa kawaida katika Milki ya Roma

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Ramani ya uenezi wa lugha za Kirumi za leo zilizotokana na Kilatini.

Kilatini kilikuwa lugha hai takriban kati ya miaka 500 KK na 600 BK na baadaye lahaja zake mbalimbali ziliendelea na kukomaa kuwa lugha za pekee zinazojulikana kama lugha za Kirumi, kama Kiitalia, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania n.k.

Kilatini ni pia jina la mwandiko au aina ya herufi (alfabeti ya Kilatini) inayotumika kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa Wikipedia.

Kilikuwa

Hadi leo Kilatini ina athira kubwa katika lugha ya sayansi na elimu. Hadi leo hufundishwa mashuleni hasa Ulaya. Tena ni

Urithi wa Kilatini katika Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]

Kiswahili kimerithi maneno yenye asili ya Kilatini hasa kupitia Kiingereza kilichopokea karibu asilimia hamsini ya maneno yake yote kutoka Kilatini kupitia hasa Kifaransa. Maneno mengine ya Kilatini yameingia Kiswahili kupitia Kireno, Kifaransa n.k.

Mifano:

Kilatini cha kisasa

[hariri | hariri chanzo]
Systema Naturae ni kitabu maarufu kilichoandikwa mnamo mwaka 1735 kwa Kilatini na Carl Linnaeus. Ni msingi wa uainishaji wa kisayansi wa mimea na wanyama hadi leo

Kilatini kilikuwa na upanuzi mkubwa kuanzia karne ya 16; misingi ya sayansi ya kisasa ilijadiliwa katika Ulaya kwa Kilatini kilichokuwa lugha ya vyuo vikuu kote Ulaya. Katika karne ya 18 na 19 mataifa mengi yaliimarisha lugha zao na kuzitumia kwa ngazi zote za elimu. Lakini wataalamu wa Ulaya na Marekani waliendelea kutumia majina ya Kilatini kwa kutaja habari za kisayansi na kubuni majina mapya kufuatana na kanuni za Kilatini kwa kutaja vitu na viumbe vilivyotambuliwa na kuelezwa kisayansi. Kazi hii iliendelea hata wakati matumizi ya Kilatini kama lugha ya kujadiliana yalishafikia mwisho wake.

Katika karne ya 20 kulikuwa na harakati ya wapenzi wa lugha kuunda misamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa, mtandao n.k. Wikipedia ya Kilatini ilifikia makala zaidi ya 130,000 kwenye mwaka 2019.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kilatini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.