Nabii Nahumu
Nabii Nahumu (kwa Kiebrania נחום, yaani "Aliyefarijiwa na Mungu") alikuwa nabii mjini Yerusalemu katika karne ya 7 KK, wakati wa mfalme Yosia, aliyetawala Yuda kati ya mwaka 640 KK na 609 KK.
Mahubiri yake yanatunzwa katika Kitabu cha Nahumu ambacho ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya gombo la Manabii wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.
Kinashangilia kwa ufasaha wa kishairi ujio wa maangamizi ya dola la Waashuru na ya makao yao makuu, Ninawi (612 KK): hivyo maadui wa taifa na wa Mungu hatimaye wataadhibiwa.
Kitarehe kinashika nafasi kati ya kile cha nabii Mika na kile cha Habakuki.
Tangu kale Nahumu anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Desemba[1][2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Nahum article from The Catholic Encyclopedia
- Renovation - Al Qush Synagogue and the Tomb of Nahum Archived 24 Agosti 2011 at the Wayback Machine.
- Prophet Nahum Orthodox icon and synaxarion
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nabii Nahumu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |