Hanani
Mandhari
Hanani (kwa Kiebrania חנני, Ḥănānî, maana yake: "YHWH amefadhili"; alizaliwa karne ya 10 KK) alikuwa nabii nchini Israeli katika karne ya 9 KK.
Alikuwa baba wa nabii Yehu na inafikiriwa kwamba waliishi kusini[1] .
Chanzo kikuu cha historia yake ni Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati, sura ya 16[2] .
Kadiri ya kitabu hicho, alimlaumu mfalme wa Yuda Asa kwa kufanya agano na mfalme wa Shamu Ben-Hadad I. Kwa ajili hiyo alifungwa na Asa bila kujali malalamiko ya wafuasi wa nabii huyo.
Wengineo
[hariri | hariri chanzo]Katika Biblia ya Kiebrania kuna watu wengine watatu wenye jina hilohilo:
- Mmoja kati ya wana wa Heman (1 Nya 25:4, 25).
- Kuhani wa familia ya Immer aliyeoa mwanamke wa mataifa (Ezr 10:20).
- Ndugu wa Nehemia ambaye alimuarifu kuhusu hali mbaya ya Yerusalemu akakabidhiwa naye malango ya mji huo (Neh 1:2; 7:2).
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Exell, J. and Spence-Jones, H. (eds.), Pulpit Commentary on 1 Kings 16, accessed 27 October 2017
- ↑ Barnes, W. E. (1899), Cambridge Bible for Schools and Colleges on 2 Chronicles 16, accessed 2 May 2020
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hanani kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |