Nenda kwa yaliyomo

Neria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Neria ni filamu ya Zimbabwe iliyotengenezwa mwaka 1993 kwa kuandikwa na Tsitsi Dangarembga na kuongozwa na Godwin Mawuru, Muongozo wa filamu uliandikwa na Louise Riber.[1]

Filamu hii ilikuwa inazungumzia mapambano ya mwanamke katika kujitafutia kipato pamoja na haki zake katika mji wa Harare mara baada ya mume wake kufa katika ajali ya kugongwa na gari,baadae kaka wa marehemu mume wa Neria anaamua kutumia nafasi ya kifo cha mdogo wake kutumia urithi kwa manufaa yake binafsi na kuwatelekeza Neria na watoto wake wawili.

Wimbo wa Neria ni wimbo ambao umekuwa ukitumika sana nchini Zimbabwe.[2] wimbo wa Neria ndani ya filamu umeimbwa na Oliver Mtukudzi.

Filamu inaanza Neria pamoja na mume wake Patrick wakipaka rangi kuta ya nyumba yao huku watoto wao wakicheza karibu,muda mfupi Patrick akionekana kuwa mwenye furaha anaaga familia yake na kuondoka,mama mkwe wake na Neria aliyekuwa amekaa karibu anaanza kumuita Neria na kumuulizia mtoto wake yaani Patrick na Neria anamwambia kuwa Patrick ameondoka muda mfupi uliopita,mama mkwe wa Neria anaanza kulaumu kuwa Neria siyo mke mwema kwa mtoto wake kwa sababu asingemruhusu kuondoka bila ya kumuaga mama yake.

Wahusika

[hariri | hariri chanzo]
  1. "From Neria to Zollywood: The State of Zimbabwean Film", eZimbabwe, 7 September 2013.
  2. Kempley, Rita. "'Neria' (NR)", 1993-04-09. Retrieved on 2007-04-15. 
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neria kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.