Dominic Kanaventi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dominic Kanaventi ni mwigizaji wa filamu na mtumbuizaji jukwaani kutoka Zimbabwe.

Filamu kadhaa alizowahi kuigiza ni pamoja na Shamwari mnamo mwaka 1982, Mandela mnamo mwaka 1987, Cry Freedom mnamo mwaka 1987 na The Midday Sun mnamo mwaka 1989. Pia alikuwa uhusika Zaidi ya moja kwenye filamu ya Neria iliyoachiliwa mwaka 1993 na Salone ya Mwaka 2016. Pia alikuwa rais wa chama cha filamu Zimbabwe ijulikanayo kama Zimbambwe Actors Guild (ZAG).

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Kanaventi alianza kama mtumbuizaji jukwaani. Mwanzoni alikuwa kama mjumbe wa kituo cha Maigizo kilichofadhiliwa na Kanisa la Katoliki kijulikanacho kama , The Mabvuku Youth Centre. [1] . Katika filamu alikuwa mhusika mkuu katika filamu ya Neria na mnamo mwaka 2001 akiigiza Zaidi ya filamu 14. .[2]

Akiwa kwenye mahojiano na Alan Tempest katika jarida la “The Standard”, alizungumza na kusema kuwa kuanzia mwezi Januari mwaka 2001 atakuwa hana uraia wa nchi maalum. Hii ilitokea kwa kuwa baba yake ni mzawa wa Msumbiji, aliweza kutembea mpaka Salisbury Rhodesia au Salisbury kama kilivyoitwa kwa kipindi hicho na ndipo alipokutana na mama yake na kumuoa. Kaventi alizaliwa mnamo mwaka 1950. [3]. Kwa matokeo ya kutokuwa na uraia wa nchi maalum, Kaventi alikwenda Marekani mnamo mwezi Februari mwaka 2002. Huko Marekani alifanya kazi kama Muuza samani na kazi ya kuuza magari huku akikamilisha na kuwa raia kamili wa Marekani mnamo mwaka 2009. Alipata stashahada ya kwanza ya utawala masoko mnamo mwaka 2014. Alifanikiwa kuanzisha kampuni yake ya kwanza inayohusika na Ushauri wa kibiashara. .[4]. Katika mahojiano mengi alisikika akisema anampenda sana mjukuu wake, Julian!

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Jukwaa[hariri | hariri chanzo]

Kama muigizaji wa jukwaani, yeye pamoja na Walter Muparusa waliweza pata tuzo ya muigizaji bora mnamo mwaka 1983, chini ya mzalishaji Andrew Whaley. .[5]. Kazi zingine aliwahi shirikiana na Ben Sinbenke mnamo mwaka 1985 katika mchezo wa kuigiza, mchezo wa maigizo huo ulijulikana kama, Sizwe Banse is Dead, mchezo wa Sanaa maarufu sana nchini Zimbabwe. [6] Katika mchezo wa mwaka 1997 ‘’Platform Five”, ikiwa ni mchezo unaohusu wazururaji na maisha yao jijini Harare, Kanaventi na Walter Muparusa walivaa kama wazururaji na walikwenda katika eneo na kukutana na watu na kujua namna gani watu wa vijijini wanavyoishi na namna maisha yao yalivyo. .[7]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Kanaventi alionekana katika filamu ya The Midday Sun kilichoachiwa mnamo mwaka 1989 na The Power of One (film)|The Power of One kilichoachiwa mwaka 1992. .[8]. Katika filamu yay a Neria, Kanaveti alicheza kama Phineas, shemeji mchoyo na mchafu, pale baada ya kifo cha kaka yake, alimfanya mjane wa marehemu kujutia. [9]. Uchezaji wake ulikuja tambuliwa na jarida ya “The Standard”. .[10]

Sanaa na Filamu[hariri | hariri chanzo]

Films Actor
Jina uhusika Muongozaji mwaka Notes #
Shamwari (film)|Shamwari Mlinzi Kiongozi Clive Harding 1982
Mandela (1987 film)|Mandela Kiongozi Philip Saville 1987 Filamu ya Runinga
Cry Freedom Polisi mtetezi wa Waafrika Richard Attenborough 1987
The Midday Sun Anthony Kacula Lulu Keating 1989
The Power of One (film)|The Power of One John G. Avildsen 1992 [11]
Neria Phineas Godwin Mawuru 1993
Salone Loyola Aswar Rahman 2016
Television Actor
Jina Kipande Uhusika Kiongozi Mwaka Notes #
Kongo 1959-1960 Partijman 1997
The Knock Episode #3.2 Kamano Geoff Harris

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Theatre and Performance in Zimbabwe, Martin Rohmer - Page 57
  2. Zimbabwe's Cinematic Arts: Language, Power, Identity, By Katrina Daly Thompson - Page 219
  3. The Standard - Zimbabwe: Kanaventi-Stateless By 2002 By Alan Tempest
  4. Western Governors University, 3/07/2016 - Different Country, Different Rules: A Cultural Education
  5. Almasi Collaborative Arts - Walter Lambert Walter Dehwe Muparutsa, The Beginning Archived 4 Februari 2021 at the Wayback Machine.
  6. Who's who in Contemporary World Theatre, edited by Daniel Meyer-Dinkgräfe - Page 279 Sibenke, Ben (1945-)
  7. Making People's Theatre, Robert Kavanagh - Page 21
  8. Zimbabwe's Cinematic Arts: Language, Power, Identity, By Katrina Daly Thompson - Page 219
  9. The Zimbabwe Herald, March 4, 2016 - Neria role swallowed Jesesi Mungoshi for five weeks
  10. The Standard.co.zw, June 2, 2013 - Arts industry poorer without Godwin Mawuru
  11. Zimbabwe's Cinematic Arts: Language, Power, Identity, By Katrina Daly Thompson - Page 219