Eberi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eberi (kwa Kiebrania עֵבֶר) ni jina la mhusika katika Biblia anayetajwa katika orodha ya mlango wa 10 wa kitabu cha Mwanzo; alikuwa mwana wa Sela na mjukuu wa Shemu, mwana wa Nuhu.

Wana wake walikuwa Pelegi na Yoktani. Kufuatana na Mwa 11:17 Eberi alimzaa Pelegi alipokuwa na umri wa miaka 34 baadaye aliishi miaka 430 akizaa wana na mabinti.

Kufuatana na mapokeo ya Kiyahudi Eberi alikufa alipokuwa na umri wa miaka 464 wakati Yakubu alikuwa na miaka 20.

Wayahudi wanamheshimu kama babu wa Abrahamu. Mara nyingi jina lake linatajwa kama asili ya neno "Waebrania" na hivyo pia asili ya lugha ya "Kiebrania".

Katika visa vya Wayahudi Eberi alikataa kushiriki katika ujenzi wa mnara wa Babeli. Kwa hiyo lugha yake haikuchafuliwa jinsi ilivyotokea kwa lugha ya hao walioshiriki katika ujenzi huo. Kufuatana na masimulizi hayo lugha ya Eberi, yaani Kiebrania ,imebaki kama lugha asilia ya binadamu wote.

Katika Hesabu 23:24 Eberi ni pia jina la dola au milki inayotajwa katika utabiri wa Balaamu kuwa, pamoja na Ashuru, itashambuliwa na merikebu kutoka Kitimu.

Katika maandiko wa Kiyahudi Eberi hutazamwa kama mmoja kati ya manabii wa kwanza aliyeendelea kufundisha Abrahamu na Yakobo. Wakati mwingine anatazamwa kama nabii anayetajwa katika Qurani kwa jina la Hūd.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eberi kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.