Nenda kwa yaliyomo

Ashuru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ashuru (ebr. אַשּׁוּר ) ni jina la mtu katika kitabu cha Mwanzo cha Biblia.

Kufuatana na masimulizi ya Mwanzo 10:11 alikuwa mwana wa pili wa Shemu mwana wa Nuhu. Kaka zake waliitwa Elamu, Arfaksadi, Ludi na Aramu[1].

Hakuna taarifa katika Biblia kuhusu ukoo wa Ashuru.

Ashuru ni pia jina la mji wa Ashuru na milki ya Ashuru na maeneo yao.

Katika Mwa. 10:11 haieleweki vizuri kama jina "Ashuru" linamtaja mtu au mji[2]. Matoleo ya Biblia kwa lugha mbalimbali zinatafsiri tofauti hapa.

  1. Mwa 10:22 : "Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. "
  2. Mwa 10:11 "Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala ..." - hii ni tafsiri ya "Biblica" ambayo katika aya hii inashika vizuri namna ya lugha ya Kiebrania isiyosema wazi kama mtendaji wa aya iliyotangulia (=Nimrodi) anakwenda Ashuru (=Mahali) anapojenga Ninawi, au kama ni mtu kwa jina la Ashuru anayetoak mahali palipotajwa awali na kujenga Ninawi