Nenda kwa yaliyomo

Inno e Marcia Pontificale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Inno e Marcia Pontificale ni Wimbo wa Taifa wa Vatikani.

Muziki wake ulitungwa -bila maneno- mnamo mwaka 1869 na Charles Gounod kwa ajili ya sikukuu ya Papa Pius IX kuwa kasisi tangu miaka 50. Uliitwa "Marche pontificale" (Kifaransa kwa "Muziki wa kimaandamano kwa Papa").

Mwaka 1949 Papa Pius XII aliutangaza kuwa muziki rasmi wa Vatikani.

Wakati ule mpigakinanda wa Vatikani, Antonio Allegra (19051969) alitunga maneno kwa muziki katika lugha ya Kiitalia kama ifuatavyo:

Roma immortale di Martiri e di Santi,
Roma immortale accogli i nostri canti:
Gloria nei cieli a Dio nostro Signore,
Pace ai Fedeli, di Cristo nell'amore.

A Te veniamo, Angelico Pastore,
In Te vediamo il mite Redentore,
Erede Santo di vera e santa Fede;
Conforto e vanto a chi combatte e crede,

Non prevarranno la forza ed il terrore,
Ma regneranno la Verità, l'Amore.

(tafsiri)
Ewe Roma ya milele, ya wafiadini na watakatifu,
Roma ya milele, pokea nyimbo zetu
Utukufu kwa Mungu, Bwana wetu mbinguni
Amani kwa waumini kutoka Kristo katika upendo.

Tunakuja kwako, ewe mchungaji wa kimalaika,
Katika wewe twamwona Mwokozi mpole
Mrithi mtakatifu wa imani ya kweli na takatifu
Mfariji na kimbilio kwa wanaopigania imani

Mbavu na tishio hazitashinda
lakini ukweli na upendo vitatawala